MSEMAJI ALIYEBADILISHA MAUMIVU KUWA ISHARA YA MAPAMBANO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ni Januari 2022, upepo wa mabadiliko ukapuliza ndani ya Msimbazi, Wakati mashabiki wengi wakijiuliza nani atachukua mikoba ya Haji Manara kwenye kuitetea nembo ya Mnyama, jina moja likaanza kunong’onwa mitaani Ahmedy Ally Wengi walimfahamu kama yule mchambuzi hodari wa michezo kutoka Azam TV, mwenye ufasaha wa maneno na sauti iliyojenga heshima katika ulimwengu wa kandanda Lakini hakuna aliyejua kuwa ujio wake Simba SC ungeibua upepo mpya wa utambulisho, umoja na mapenzi ya dhati kwa klabu hiyo kongwe.

Ahmedy Ally hakujiunga Simba kama kiongozi tu, bali kama mwanaharakati wa soka pale msimbazi, tangu siku ya kwanza, alijitosa katikati ya mashabiki, akizungumza nao kwa lugha yao, akiwapa matumaini hata pale ambapo matokeo hayakuwa rafiki. Katika nyakati za kupoteza mechi, alipaza sauti ya faraja akiwakumbusha kuwa “Simba ni zaidi ya klabu barani Afrika yenye heshima na historia ya kipekee" .

Lakini safari haikuwa rahisi Simba SC ilipitia misimu migumu, ikikosa taji la Ligi Kuu mara nne mfululizo ikichagizwa na kipigo mara tano mfululizo dhidi ya mtiani wao Yanga SC hali iliyotikisa mioyo ya mashabiki wengi. Wakati baadhi walikatishwa tamaa, Ahmedy Ally alisimama imara kama nguzo ya matumaini, Kwa sauti yake tulivu lakini thabiti, aliendelea kuwahamasisha mashabiki kuamini katika klabu yao akisisitiza kuwa kila kipigo ni somo, na kila msimu ni nafasi mpya ya kurudi kwa kishindo.

Kila baada ya mechi ngumu, Ahmedy hakuwa msemaji wa visingizio, bali alikubali uhalisia na kukiri udhaifi huku akitoka maneno yenye faraja na mizaha ndani yake ambayo yanakuwa ni faraja kwa Simba Sc , huku akiwa bingwa wa misemo mfano "Ubaya ubwela' Kauli hizo ziliendelea kuwa dira ya mashabiki waliokuwa wakihitaji sauti ya faraja na kuunganishwa tena na klabu yao.

Na sasa, akiwa mstari wa mbele kuongoza operesheni kabambe ya kukomesha uuzaji wa jezi feki, Ahmedy ameonyesha upande mwingine wa uongozi wake ule wa utendaji na uzalendo wa kiuchumi kwa klabu ya Simba Ameshika bango la mapambano akisisitiza kuwa kila jezi halali ni sauti ya mabadiliko, ni njia ya kumsaidia mchezaji na kuinua mapato ya klabu.

Kwa hakika, Ahmedy Ally amekuwa nguzo ya utambulisho wa kisasa wa Simba SC, akiiweka klabu hiyo katika hadhi ya kimataifa bila kuisahau mizizi yake ya jadi. Kwa maneno yake makini, kwa kazi yake ya moyo, na kwa bidii yake isiyopungua, ameibeba Simba mabegani si kama kiongozi wa ofisini, bali kama mwana Simba wa damu.

Ama kweli Ahmedy sio tu msemaji ni mwanaharakati wa soka aliyejitoa muhanga kuhakikisha klabu ya Simba inabaki kwenye hadhi yake licha ya changamoto zitakazo jitokeza amakweli anacho kufanya Ahmed ni uzalendo wa kweli misiri ya mtu aliekunywa maji ya bendera,

HAKIKA WA SIMBA WANATAKIWA KUANDAA KEKI KWA AHMEDY ALLY KAMA SHUJAA WA TIMU YAO.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments