MSAIDIZI WA FOLZ ATAMBULISHWA JANGWANI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Yanga Africans imemtambuliasha Patrick Mabedi raia wa Malawi kuwa kocha msaidizi klabuni hapo ambapo amekuja kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi akishirikiana na kocha mkuu Romain Folz.

Mabedi anaumri wa miaka (51) amewahi kuwakocha mkuu timu ya Taifa ya Malawi na msaidizi kwenye klabu kubwa kama Kaizer Chief, hivyo anauzoefu wa kutosha katika benchi la ufundi.

HIZI HAPA BAADHI YA TIMU ALIZOWAHI KUZINOA

2016-2017- kocha mkuu Cape town All Stars

2017-2018- Kocha msaidizi Kaizer Chief

2019 - Black- leopards

2020-2023 - Malawi U-20

2023-2025 - Malawi senior

Huu ni uzoefu alionao kocha Mabedi na nimatumaini ya Wananchi kuwa atashilikiana vyema na benchi la ufundi chini ya kocha Folz kuhakikisha timu inaimarika kiuchezaji na wanakamilisha malengo ya timu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments