MMADAGASCAR ATEMWA, FOLZ KUBAKI JANGWANI

 

Timothy Lugembe

Mwanakwetusports.

Baada ya mjadala wa muda mrefu kuhusu mustakabali wa kocha mkuu wa Yanga Africans Romain Folz hatimaye majibu yamepatikana baada ya kikao Cha viongozi wa klabu kuwa kocha huyo ataendelea kuinoa klabu hiyo huku ikiarifiwa kuwa ataongezewa msaidizi ili kuhakikisha benchi la ufundi linaimarika.

Taarifa za awali zilisema kuwa kocha wa timu ya Taifa Madagascar Romuald Rakotodrabe angechukua mikoba ya Folz klabu hapo baada ya kuwa tayali alisha tumiwa ofa na kilicho kuwa kimebaki ni yeye kujiunga na miamba hiyo lakini mchakato umekwama baada ya maamuzi ya kikao.

Hata hivyo klabu itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa timu ikiwa na maana kuwa kama hawataridhishwa na kiwango cha uchezaji chini ya kocha huyo bas maamuzi magumu yatafanyika ikiwemo kumfungashia virago.

Kilicho pelekea kocha huyu kutaka kutimuliwa klabuni hapo sio kutopata matokeo bora bali uchezaji usiiridhisha mashabiki na viongozi wa timu hiyo wanahitaji timu icheze mpira wa kuvutia na kupata matokeo kwa ushawishi, hii itabidi kocha huyo kubadilisha falsafa zake kiuchezaji ili kukidhi matakwa ya mashabiki na viongozi.

Je, kumlazisha kocha kutoka nje ya falsafa zake Ina afya kimpira? huenda kocha huyu akafuata wanachokililia mashabiki na viongozi na bado wakapata matokeo yasiyo bora, ni vizuri kama walikuwa hawaridhishwi na uchezaji wa kocha huyu wangesimamia maamuzi ya kumbadili na sio yeye abadili falsafa zake kiuchezaji.

0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments