Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu tisa kutoka Barani Afrika zimejihakikishia nafasi zao za kushiriki Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika Marekani, Mexico na Canada, baada ya kumalizika kwa michezo ya kufuzu mwishoni mwa wiki.
Timu zilizofanikiwa kufuzu moja kwa moja ni Morocco, Tunisia, Algeria, Misri, Ghana, Cape Verde, Afrika Kusini, Ivory Coast na Senegal, ambazo zimeongoza makundi yao , huku timu za Gabon, DR Congo, Cameroon na Nigeria zikisubiri play off ilikupata timu moja itakayo enda kucheza mtoano dhidi ya timu kutoka mashirikisho mengine Duniani ( inter Confederation play off).
Michezo ya play off itapigwa Novemba 13-16 mwaka huu nchini Morocco ambapo Nigeria atakutana na Gaboni, huku Cameroon akikutana na Congo DR, mchezo ukiwa ni wa mkondo mmoja kwa Kila hatua (single leg) , mshindi katika hatua hiyo ataenda Moja kwa Moja kucheza mtoano na timu kutoka mashirikisho mengine.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment