Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Meneja mpya wa klabu ya Simba Sc Dimitar Pantev ameianza safari yake vyema katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal kutokea Sudani kwa kuibuka na ushindi wa 2-1 kwenye dimba la Meja Jenerali Isamuhyo.
Waliosherehesha mchezo huo kwa mabao upande wa Simba alikuwa ni Jean Ahoua na Jonathan Sowah huku bao la kufutia machozi kwa Al Hilal likikwamishwa kimiani na Adama coulibaliy.
Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza Pantev klabuni hapo na tayali kashaanza kuonyesha makali, Wana Simba wanatarajia makubwa zaidi kutoka kwake ikiwemo kuwafikisha hatua za juu kimataifa na Kutwaa ubingwa wa ligi kuu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment