Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports,
Klabu ya Simba SC inakabiliwa na changamoto kuelekea mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini, utakaochezwa Jumapili, Oktoba 19, baada ya nyota kadhaa muhimu kukosekana kwenye msafara huo.
Mlinda mlango wa kimataifa wa Guinea, Moussa Camara, hatakuwa sehemu ya kikosi hicho baada ya kushindwa kupona kikamilifu kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali dhidi ya Gaborone United.
Pia, Mohamed Bajaber hatakuwa sehemu ya kikosi hicho licha ya kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake, wakati Abdurazack Hamza naye ataendelea kukosekana kutokana na jeraha alilopata katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC.
Kwa upande mwingine, kiungo fundi Allasane Kanté naye hatasafiri na kikosi hicho kutokana na maumivu madogo aliyoyapata mazoezini, hatua itakayomfanya Kocha Mkuu kutegemea zaidi wachezaji chipukizi na wale waliopo kwenye hali nzuri kiafya.
Simba SC wanatarajia kupambana na Nsingizini Hotspurs wakisaka matokeo mazuri yatakayowawezesha kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakiwa na matumaini makubwa ya kurejea Tanzania wakiwa na matokeo chanya licha ya kukosa nyota wao muhimu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment