MASHETANI WEKUNDU WAFANYA BALAA , MAJOGOO WAPIGIKA MARA NNE MFULULIZO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezo wa mahasimu wakubwa ligi kuu nchini Uingereza uliowakutanisha Liverpool dhidi ya Manchester United katika dimba la Anfield umetamatika kwa mashetani wekundu kupata utukufu wa 2-1 katika uwanja wa ugenini.

Katika mchezo huo Livepool waliumiliki mpira kwa muda mrefu huku walipiga mashuti 19 na sita pekee yakilenga lango na kuzalisha bao Moja kupitia kwa Gakpo 78' huku United wakipiga mashuti 14 na manne yakilenga lango na kuzalisha mabao mawili yaliyofungwa kupitia Mbeumo 2' na Maguire 84'.

Hii ni mara ya kwanza kwa United kupata ushindi dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield toka mwaka 2016 ambapo Wayne Rooney ndio alipeleka furaha Old Trafford imepita miaka Tisa na mwiko huo umevunjwa.

Unakuwa ni mchezo wa nne mfululizo kwa livepool kupoteza katika michezo ya kimashindano huku hali yao inadhidi kudhoofika baada ya kushushwa mpaka nafasi ya nne na Arsenal akiendelea kujikita kileleni .

Ishara mbaya kwa majogoo ilianza kuonekana baada ya kujenga tabia yakushinda dakika za mwishoni , kwa sasa wameanza kupoteza michezo mfululizo na kuanza kupoteza matumaini ya kufanya vizuri wakiwa wanazidi kushuka kwenye msimamo.

Ligi kuu nchini Uingereza imekua haitabiriki kufanya vibaya kwa Liverpool hakujaondoa matumaini yakutetea ubingwa wao , muda wowote msimamo unaweza kubadilika kwa kuzingatia tofauti yao na Arsenal na alama tano.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments