MADRID YAKATAA UTUMWA KWA BARCELONA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports

Kabla ya mchezo wa El clasico hapo Jana Kila mmoja alikuwa anajiuliza ni lini Real Madrid watajikomboa na utumwa kutoka Kwa vijana wa Barcelona, na Wengi wakiamini kuwa vipaji vya FC Barcelona vingeweza kuwatesa wapinzani wao lakini mambo yalikwenda ndivyosivyo.

Mchezo huo uliopigwa dimba la Santiago Bernabeu nyumbani kwa madrid ambapo minyonyoro ya utumwa ilikatwa na ushindi wa 2-1 kupitia kwa Kylian Mbappe 22' na Bellingham 43' huku Lopez akipunguza machungu dakika ya 38'. Katika mchezo huo ilishuhudiwa kadi nyekundu kwa Pedri 99+9.

Huu unakuwa ushindi wa kwanza kwa madrid baada ya kupitia mateso mara tano mfululizo kutoka kwa wapinzani wao na kwa ushindi huo wanajikita kileleni kwa tofauti ya alama tano wakiwa na alama 27 huku Barcelona wakisalia na alama 22 baada ya michezo 10.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com




0/Post a Comment/Comments