LALIGA , EPL LIGI ZIMEKOLEA NAZI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ligi kuu nchi uingereza na Hispania zimezidi kuwa na ushindani wa hali ya juu baada ya matokeo ya yasiyotarajiwa kwa vigogo kuangusha alama na kupoteza nafasi zao huku mvuto wa kiushindani katika ligi hizo ukiongezeka.

EPL- ligi kuu Uingereza

Michezo ya mzunguko wa Saba katika ligi hiyo iliopigwa huku ilishuhudiwa klabu ya Liverpool ikipoteza dhidi ya Chelsea kwa 2-1 huku ukiwa ni mchezo wa tatu mfululizo wakipoteza mara baada ya kufungwa na palace, Galatasaray katika UEFA na wikendi hii.

 kipigo dhidi ya Chelsea kimewaporomosha kutoka kileleni hadi nafasi ya pili huku Arsenal wakipata ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham nakuwafanya wakwee kileleni kwa tofauti ya alama Moja dhidi ya Liverpool wakiwa na alama 16.


LALIGA- Ligi kuu nchini Hispania

Katika michezo ya mzunguko wa nane katika ligi kuu nchini Hispania imeendeleza kutimua vumbi huku ikiwa na matokeo ya kushangaza baada ya klabu FC Barcelona kupoteza kwa kipigo Cha 4-1 dhidi ya Sevilla wakiwa ugenini ambapo wapinzani wao wakubwa klabu ya Real Madrid wakiipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Villarreal.


 Kwa matokeo hayo Barcelona wameshuka kileleni wakibaki na alama 19 huku Madrid wakikwea kileleni kwa tofauti ya alama Moja wakiwa na alama 20 ikumbukwe huu unakuwa ni mchezo wa pili mfululizo wanapoteza mara baada ya kupoteza dhidhi ya PSG kwa kufungwa 2-1 kwenye UEFA champions league.

Ligi hizo zimekuwa na ushindani mkubwa baada ya tofauti ya alama baina ya timu ya kwanza na zinafuata kuwa na pengo dogo huku nafasi ya kwanza na  timu zinazofuata zikipishana kwa alama chache kitu ambacho kinaongeza radha ya kiushindani katika ligi hizo.



Kwa matokeo na mwenendo huo tutarajie makubwa zaidi kuelekea kumpata bingwa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments