KOCHA WA MOROCCO: WENYEJI WA AFCON HAWABEBI TAJI KIRAHISI


 Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui, ameibua mjadala mzito baada ya kudai kuwa mara nyingi mataifa yanayoandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) huishia kushindwa kutwaa ubingwa huo.

 Akizungumza na vyombo vya habari nchini humo, Regragui alisema historia inaonesha ni wachache waliowahi kubeba taji hilo wakiwa wenyeji.

“Mataifa makubwa kama Misri, licha ya ubora wao mkubwa kisoka, yameshindwa mara kadhaa kutwaa taji hilo nyumbani,” alisema kocha huyo wa Morocco ambaye timu yake ndiyo mwenyeji wa michuano ijayo ya AFCON.

Kauli hiyo imezua gumzo kubwa miongoni mwa wadau wa soka barani Afrika, huku baadhi wakiamini Regragui anajaribu kupunguza shinikizo kwa wachezaji wake kabla ya mashindano hayo makubwa.


Hata hivyo, wengine wameitafsiri kauli hiyo kama ishara ya hofu na kutokuwa na imani na uwezo wa Morocco kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kutwaa ubingwa huo. Mashabiki wengi sasa wanangoja kuona kama taifa hilo litavunja “laana” ya wenyeji kushindwa kutwaa taji la AFCON.

Lakini kauli hii nikama haiana mashiko ukizingatia kwa Afrika timu mwenyeji ndio ana nafasi kubwa kutokana na faida ya mashabiki, mashindano ya AFCON yaliyopita timu ya Taifa ya Ivory cost walitwaa ubingwa wakiwa nyumbani , swali ni kwanini kocha huyo anatoa kauli za kutojiamini wakati timu yake ndiyo inapewa nafasi kubwa.

Acha tuichukue kauli hii kama mbinu ya kiufundi ya kupunguza shinikizo kwa wachezaji na mashabiki na sio kwamba ni kweli hawana uwezo wa Kutwaa ubingwa wakiwa nyumbani ukilinganisha na kikosi Bora zaidi barani Afrika.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments