Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Dar es Salaam imewaka moto kwa tetesi baada ya kocha maarufu, Nasreddine Naby, kutua nchini na kuibua gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka taarifa za ndani zinaeleza kuwa huenda Naby akatangazwa kuwa kocha mpya wa moja ya miamba ya soka ya Kariakoo Simba SC au Yanga SC muda wowote kuanzia sasa.
Naby, ambaye ana rekodi nzuri katika soka la Afrika, amewasili nchini huku kukiwa na matumaini kumalizana na uongozi wa moja ya vigogo hao, hali ambayo imezidisha minong’ono mitaani na mitandaoni , Mashabiki wa Simba na Yanga kwa pamoja sasa wana hamu ya kufahamu ni je, ni klabu ipi imefanikiwa kumshawishi kocha huyo.
Miamba hiyo miwili ya Kariakoo imekuwa katika harakati za kuimarisha benchi la ufundi kuelekea msimu mrefu wa mashindano ya ndani na kimataifa. Hali hii imefanya ujio wa Naby kuwa gumzo kubwa, huku kila upande ukijiona una nafasi kubwa ya kumpata.
Iwapo Naby atasaini, atakuwa sehemu ya historia ya moja ya timu kubwa zaidi nchini na kuendelea kuongeza mvuto wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo kwa sasa imekuwa kivutio kikubwa barani Afrika.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment