Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Tetesi zilizoenea kwa muda mrefu kuhusu kocha mpya wa Simba SC hatimaye zimethibitishwa rasmi, Vigogo hao wa Kariakoo wamekamilisha usajili wa kocha Dimitar Nikolaev Pantev, raia wa Bulgaria, ambaye amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili hadi Juni 2027.
Pantev, mwenye umri wa miaka 49, anakabidhiwa jukumu la kurithi mikoba ya benchi la ufundi la wekundu wa Msimbazi baada ya Simba kufikia makubaliano ya fidia na klabu ya Gaborone United kutoka Botswana aliyokuwa akiinoa.
Katika benchi lake, Pantev ataanza na kocha msaidizi mmoja pekee, huku mikataba ya makocha waliopo Simba ikitarajiwa kumalizika mwezi Juni,Uongozi wa klabu umeamua kumpa mamlaka ya kuamua nani ataendelea naye baada ya mwezi huo, jambo linaloonyesha imani kubwa waliyonayo kwa uwezo wake.
Safari yake ya ukocha siyo ya kawaida tayari ametwaa mataji ya ligi akiwa na Victoria United ya Cameroon na Gaborone United ya Botswana, rekodi inayompa heshima kubwa barani Afrika, Mashabiki wa Simba wanaiona hatua hii kama mwanzo wa enzi mpya ya ushindani na mafanikio makubwa.
Kwa sasa, jicho la wapenzi wa soka nchini limeelekezwa Dar es Salaam, wakisubiri kumuona “Mshindi wa kweli” huyo akianza safari yake ya kusaka mataji akiwa na wekundu wa Msimbazi.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment