KIPAJI CHIPUKIZI SENEGAL AUAWA BAADA YA KUTEKWA NCHINI GHANA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Dunia ya soka imegubikwa na simanzi baada ya kifo cha kipa kinda raia wa Senegal, Cheikh Touré (18), ambaye ameuawa nchini Ghana baada ya kutekwa na watu waliomualika kwa majaribio ya soka.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wanahabari wa michezo, Touré alipokea mualiko wa kwenda kufanya majaribio katika moja ya vilabu vikubwa nchini Ghana, akiwa na matumaini ya kuanza safari yake ya soka la kulipwa hata hivyo, ndoto hiyo iligeuka kuwa jinamizi baada ya kufika nchini humo na kutekwa na watu waliodai fidia kwa familia yake.

Inadaiwa kwamba watekaji walitaka kulipwa kiasi kikubwa cha fedha ili kumwachia kijana huyo akiwa hai, lakini familia yake haikuweza kufanikisha malipo hayo, baada ya juhudi za muda fulani, taarifa zilithibitisha kuwa Touré aliuwawa na watekaji.

Kifo cha kijana huyo kimeibua masikitiko makubwa katika jamii ya soka nchini Senegal na Afrika kwa ujumla, huku wadau wa michezo wakitoa wito kwa vyama vya soka kuweka utaratibu wa kudhibiti matapeli wanaojifanya mawakala wa wachezaji chipukizi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments