KARIA, HERSI NA NEEMA HAJI WALAMBA TEUZI FIFA

  


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limewateua viongozi kutoka Tanzania kushika nafasi katika kamati zake za kimataifa, hatua inayotajwa kuwa heshima kubwa kwa taifa na soka la Afrika Mashariki kwa ujumla.

Katika teuzi hizoFIFA imemteua Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Soka la Ufukweni ya FIFA kwa kipindi cha miaka minne hadi mwaka 2029.


Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said, ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu vya Wanaume Duniani, nafasi atakayoitumikia kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2025 hadi 2029, Uteuzi huo unamfanya Hersi kuwa mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na Kati kuingia katika kamati hiyo kubwa ya FIFA.

Vile vile FIFA imemteuwa Neema Haji kuwa mjumbe wa kamati ya mashindano kwa wasichana.

Uteuzi huu wa viongozi kutoka Tanzania umeonyesha wazi namna nchi hiyo inavyozidi kupata heshima katika ulimwengu wa soka, ikiwa ni ishara ya maendeleo na utambulisho mzuri wa michezo nchini.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments