KAIZER NA NABI IMEKWISHA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Kaizer Chief imefikia makubaliano ya pande zote mbili na alie kuwa kocha wao Nasreddine Nabi sasa hatainoa klabu hiyo kwa sasa yupo huru kujiunga na klabu yoyote.

Tayali kocha huyo amewaaga wachezaji, mashabiki na viongozi wa timu hiyo hivyo maisha yake ya ukocha yataanza upya katika timu nyingine ambayo itaonyesha nia yakuhitaji huduma yake muda wowote kuanzia sasa.

Ni mwaka mmoja na miezi miwili toka alipo kabidhiwa kuinoa klabu hiyo akiiongoza katika michezo 35 akishinda michezo 12 sare 9 na kupoteza michezo 14 na hayo ndio maisha ya Nabi alipokuwa Kaizer Kila lakheri kwenye majukumu yake mapya.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments