HIZI HAPA TUZO ZA MWEZI SEPTEMBA NBC 2025/2026


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha mkuu wa kikosi Cha JKT Tanzania Ahmad Ali ameibuka kocha Bora wa mwezi septemba wa ligi kuu NBC 2025/2026 akiwapiku Romain Folz wa Yanga Africa na Miguel Gamond wa Singida black stars.

Ahmad alikiongoza vizuri kikosi chake ambapo katika michezo miwili ya ligi aliyocheza mwezi septemba alitoa Suruhu na Mashujaa 1-1 na ushindi wa 2-1 dhidi ya Costal Union michezo yote akiwa ugenini.

Katika hatua nyingine mlinda lango wa klabu ya Yanga Djigui Diarra ameibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi septemba wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuongoza timu yake kwenye michezo miwili ambapo walipata ushindi wa 3-0 dhidi ya Pamba Jiji na sare tasa 0-0 dhidi ya Mbeya City na kutoruhusu bao katika michezo hiyo.


Diarra aliwashinda Antony Trabi wa Singida black stars na Mohamed Bakari wa JKT Tanzania ambao alichuana nao katika hatua ya fainali ya kutafuta mshindi wa tuzo hiyo.

Tuzo hizo zimetolewa na kamati ya tuzo kutoka shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments