HISTORIA YA YANGA , MBEYA CITY SOKOINE


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Baada ya mchezo kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City uliopigwa katika dimba la sokoine ulimalizika kwa sare ya bila kufunguna , baada ya wenyeji Mbeya City kuilazimisha Yanga SC sare tasa ya 0-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.


Matokeo hayo yanaendeleza rekodi ya Yanga kushindwa kuibuka na ushindi katika Uwanja huo tangu mwaka 2018, ambapo walishinda kwa magoli 2-1 kwa mabao ya Heritier Makambo, tangu hapo, kila walipokutana na Mbeya City ugenini wameshindwa kuondoka na pointi tatu.

Mara ya mwisho miamba hiyo ya soka kukutana ilikuwa Juni 06, 2023, mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3 huku ukitawaliwa presha ya juu, ikiwemo wachezaji wa Yanga, Hassan Nassor Maulid na Jesus Moloko, kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 87, baada ya kipenga cha mwisho, Yanga walikabidhiwa kombe la ubingwa wa msimu wa 2022/2023.

Kwa sare ya jana, Wananchi wanaendelea kutafuta ushindi wao wa kwanza katika ardhi ya Sokoine kwa zaidi ya miaka mitano, huku Mbeya City wakionekana kuwa mwiba mchungu kila wanapokutana na mabingwa hao watetezi.

Mashabiki wa Yanga sasa wanaanza kujiuliza ni lini mwiko huo wa kutoshinda Sokoine dhidi ya mbeya city utavunjwa, hasa ikizingatiwa timu ipo katika mbio za kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Baada ya.mchezo huo Yanga wanadondosha alama mbili wakisalia na alama nne katika michezo miwili huku Mbeya city wakiwa na alama nne katika michezo mitatu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments