Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Historia imeandikwa katika soka la Tanzania baada ya kushuhudia kwa mara ya kwanza timu nne kufuzu hatua ya makundi kwa klabu bingwa na shirikisho timu za Simba, Yanga , Azam na Singida zimekata tiketi kwa pamoja kuliwakilisha Taifa barani Afrika.
Azam fc na Singida black stars, inakuwa ni mara yao ya kwanza kutinga hatua ya makundi toka kuanzishwa kwao.
Historia hii imeandikwa kutokana na matunda ya uwekezaji katika klabu hizo ikiwemo usajili Bora kuanzia wachezaji mpaka benchi la ufundi kitu ambacho kimetoa matokeo chanya , hivyo kati ya timu 32 zilizofuzu makundi Shirikisho na klabu bingwa Afrika ,Tanzania imetoa timu nne.
Hii inamaanisha kuwa soka la Tanzania linazidi kukua na kupiga hatua kutokana na uongozi imara na ufuatiliaji wa kina pia uboreshwaji wa miundombinu ya viwanja na kusababisha wachezaji wengi wa kigeni kuvutiiwa kucheza katika ligi ya Tanzania na kuwa chachu ya mafanikio kwenye vilabu vyetu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com

.jpg)


Post a Comment