Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya Taifa ya Cape Verde imefuzu kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yake ya soka baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Eswatini nakuongoza kundi D' wakiwa na alama 23 kwenye michezo 10 waliyocheza huku nafasi ya pili ikishinwa na Cameroon wenye alama 19 kwa msimamo huo Moja kwa Moja Cape Verde wanafuzu kombe la Dunia 2026.
Hivyo, Linakuwa ni Taifa la pili kwa udogo kufuzu michuano hiyo mikubwa baada ya Iceland kufanya hivyo , cape Verde Ina raia takribani 590,000 watu wachache ukilinganisha na baadhi ya mataifa mengine.
Kwa sasa timu hiyo inajiandaa kwenda kuliwakilisha bara la Afrika kwenye michuano mikubwa zaidi ulimwenguni ikiwa ni mara yao ya kwanza na historia mpya na kubwa katika soka la nchi hiyo limeandikwa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment