Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashabiki wa soka ulimwenguni jana walishuhudia usiku wa kihistoria uliokuwa na mvua ya mabao na kadi nyekundu katika michezo mbalimbali ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo jumla ya mabao 43 yalifungwa huku kadi nyekundu tano zikioneshwa katika michezo hiyo.
Timu ya Barcelona iliichapa Olympiacos mabao 6-1, mchezo uliokuwa na kasi kubwa na mvutano kila dakika, huku refa akilazimika kutoa kadi nyekundu kwa Santiago Hezze 57' mchezaji wa Olympiacos.
Nchini Uingereza, Arsenal iliendelea kutamba kwa ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Atletico Madrid, ushindi uliowapa nguvu kubwa kuelekea hatua zinazofuata, Wakati huo huo, Newcastle United walionekana moto wa kuotea mbali baada ya kuwachapa Benfica kwa mabao 3-0 bila jibu.
Mechi iliyovutia wengi ilikuwa ni kati ya Bayer Leverkusen na PSG, ambapo mashabiki walishuhudia jumla ya mabao 9 yakifungwa, PSG wakiibuka kidedea kwa ushindi wa 7-2, kuku Robert Andrich wa Leverkusen akionyeshwa kadi nyekundu 31' na Ilya Zabarnyi wa PSG 37'.
Katika ardhi ya Uholanzi, PSV Eindhoven waliitandika Napoli kwa mabao 6-2, huku pia kadi nyekundu ikitolewa kwa mchezaji wa Napoli Lorenzo Lucca 76' .
Kwa upande mwingine, Borussia Dortmund waliibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya FC København, wakati Inter Milan walitamba kwa kishindo kwa ushindi wa 4-0 mbele ya Union St. Gilloise, na Manchester City wakihitimisha usiku huo kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Villarreal.
Huku mchezo kati ya Kairat Almaty na Pafos ukiisha kwa sare tasa huku kadi nyekundu ikionyeshwa kwa Joao Correia 4' mchezaji wa Pafos.
Mashindano hayo yatarajiwa kuendelea kutimua vumbi Leo kwa michezo tisa itakayo kwenda kukamilisha mzunguko wa tatu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment