AZAM FC WAANDIKA HISTORIA AFRIKA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabua ya Azam fc imeandika historia ya aina yake baada kufanikiwa kutinga hatua ya makundi kombe la shirikisho(CAFCC) kwa kupata ushindi wa Jumla ya mabao 9-0 dhidi ya KMKM kutokea Visiwani Zanzibar katika hatua ya pili ya wali.

Kwenye ushindi wa bao 7-0 katika dimba la Chamanzi mabao yaliwekwa kimiani na Idd Nado 23' , 43, Kitambala 23', 30, Msindo 49' na Abdul Sopu 53', 57 . Ushindi ulio kamilisha ndoto za Wana lambalamba kutinga hatua ya makundi.

Azam, imekuwa klabu yenye Kila rasilimali lakini ilikuwa ikipata shida kujitambulisha barani Afrika toka kuanzishwa kwake klabu ina miaka 21 na kwamara ya kwanza inafuzu hatua ya makundi kwenye michuano hiyo.

Haya ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Klabu hiyo kuanzia kwenye usajili wa wachezaji mpaka benchi la ufundi ikiwa na dhamira kubwa ya kutambulisha nembo ya timu hiyo barani Afrika.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments