Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa klabu ya Marseille na timu ya Taifa ya Gabon Pierre Aubameyang ameibuka nyoka kwenye mchezo wkufuzu kombe la dunia 2026, baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 4-3 wakiwa ugenini dhidi ya Gambia.
Katika mchezo huo mabao yote manne ya Gaboni yaliwekwa kambani na Aubameyang huku akisindikizwa na kadi nyekundu aliyo onyeshwa dakika ya 86' , katika mchezo huo amekuwa nguzo huku wakiendelea kushindilia matumaini ya kufuzu kombe la Dunia.
Gaboni wanashika nafasi ya pili kundi F wakiwa na alama 22 nyuma ya Ivory coast wenye alama 23 ikiwa ni tofauti ya alama Moja, umebaki mchezo mmoja ili kujua hatima Yao kama watafuzu Moja kwa Moja au watacheza play off.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment