Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Atletico Madrid Julian Alvarez, amepanga kuondoka klabuni hapo ifikapo mwaka 2026 ili kusaka changamoto na maendeleo zaidi katika tasnia yake ya soka.
Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na klabu hiyo, uamuzi wa Alvarez unatokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kuporomoka kwa kiwango cha Atletico katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, hali iliyomfanya straika huyo kuamini kuwa amekomaa zaidi ya kiwango cha timu hiyo kwa sasa.
Tangu kujiunga na Atletico Alvarez amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaoleta chachu katika La Liga, akijipatia mashabiki wengi kutokana na kasi yake, uwezo wa kupiga mipira ya mbali, na umakini mkubwa langoni.
Klabu ya Barcelona inatajwa kuwa kinara katika kumsaka mchezaji huyo, huku ikiripotiwa kuwa tayari imeanza mazungumzo ya awali na mawakala wake, hata hivyo, kiasi kinachohitajika kumvuta kutoka Madrid kinaweza kuzidi Euro milioni 150, jambo linaloweza kuwa kikwazo kwa baadhi ya vilabu vinavyomnyemelea.
Kwa sasa, macho yote yameelekezwa Madrid, wakisubiri kuona kama straika huyo wa kimataifa wa Argentina atadumu au ataamua kufungua ukurasa mpya katika historia yake ya kisoka.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment