Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports
Ligi mbali mbali barani ulaya zilishika Kasi hapo Jana huku matokeo yakushangaza yakijitokeza kwa ukubwa baada ya vigogo kuangukia pua isivyo matarajio ya mashabiki na wadau wa soka ulimwenguni kote.
Katika EPL ndipo vilio vilitawala baada ya vigogo watatu kuacha alama tatu dhidi ya wapinzani wao.
Crystal palace 2-1 Liverpool
Kwa mara ya kwanza klabu ya Liverpool inakubali kichapo baada ya kutoruhusu kufungwa katika michezo mitano nyuma ya EPL, mchezo huu uliopigwa dimba la Selhurst park mabao yaliyo wapa ushindi palace yaliwekwa kimiani na Ismaila Sarr 9' na Edward Nketiah 90+7 huku bao la kufutia machozi upande wa majogoo likifungwa na Federico Chiesa 87'. Baada ya mchezo huo Liverpool wanasalia kileleni na alama 15 huku palace wakisogea hadi nafasi ya pili na alama 12.
Chelsea 1-3 Brighton
Huu ni mchezo wa pili mfululizo kwa the blues kupoteza alama tatu baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Man utd wikend iliyopita, mchezo huu uliopigwa uwanja wa Stamford bridge ambapo Chelsea walikubali yaishe kwa kuruhusu kufungwa bao 3 ambapo Mabao yaliyo wauwa Chelsea yalifungwa dakika za nyongeza , katika mchezo huo mabao ya Brighton yalifungwa na Danny Welbeck 77' , 90+10, na Maxim de Cuyper 90+2' huku bao la the blues likifungwa na Enzo Fernandez.
Brentford 3-1 Man utd
Hali inazidi kuwa mbaya kwa klabu ya united hii inatokana na kushindwa kupata matokeo mfululizo ya ushindi baada ya kuonja radha ya ushindi dhidi ya Chelsea wikendi iliyopita wamerudi tena kwenye kipigo, katika mchezo uliopigwa katika dimba la Gtech Community stadium, Brentford waliutumia uwanja wao wa nyumbani vyema kwa kufunga bao tatu zilizo wekwa kimiani na Ignor Thiago 8' 20' na Mathias Jensen 90+5 huku bao la united likifungwa na Benjamin Sesko 26'.
Atletico Madrid 5-2 Real Madrid
Mchezo wa dabi ya Madrid uliopigwa dimba la Riyadh air metropolitano ambapo ilishuhudiwa vijana wa Simeone wakitembeza dozi kwa Real Madrid baada ya kutakata na ushindi wa bao Tano mabao yaliyokwamishwa kimiani na Robin Normand 14', Alexander Sorloth 45+3, Julian Alvarez 51' 63 na msumali wa maumivu ukimaliziwa na Griezmann 90+3. Huku mabao yakufutia maumivu Kwa vijana wa Bernabeu yalifungwa na Kylian Mbappe 25' na Arda Guler 36'.
Kwa matokeo hayo mwenendo wa ligi umebadilika huku mapengo ya alama yakipungua na kuongeza ushindani kwa EPL baada ya Liverpool kupoteza pengo limepungua kutoka alama Tano Hadi alama tatu dhidi ya anayemfuatia, huku pale Laliga Madrid anatarajia kushushwa kileleni iwapo Barcelona watapata ushindi , hivyo vipigo hivyo vimebadilisha taswira na mwenendo wa ligi .
Tunaweza kusema ligi zimechanganya tutarajie kuona ushindani wa aina yake.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment