Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba Sc imeadhibiwa na shirikisho la mpira barani Afrika CAF kutoingiza mashabiki kwenye mchezo wake wa marudiano mzunguko wa kwanza dhidi ya Gaborone united ya Botswana mchezo utakaopigwa septemba 28 mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa.
Ikumbukwe msimu uliopita katika mashindano ya shirikisho, klabu ya Simba iliadhibiwa kutoingiza mashabiki kwenye mchezo dhidi ya Constantine mara baada ya mashabiki wake kufanya vurugu kwenye mchezo dhidi ya Cs Sfaxien na katika adhabu hiyo iliendelea kuwa iwapo watarudia kosa ndani ya miezi 12 watafungiwa tena.
Katika mchezo wa robo fainali kombe la shirikisho dhidi ya Al Massry klabu hiyo ilirudia tana makosa baada ya shabiki wake kuingia uwanjani na kuleta vurugu huku kosa lingine likiwa ni kuwasha Moshi uwanjani( Moshi mwekundu wanaowasha mashabiki wa Simba wakiwa wanashangilia).
Kwa makosa hayo klabu ya Simba haitaingia na mashabiki kwenye mchezo wao mkondo wa pili dhidi ya Gaborone united.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment