THE SPECIAL ONE KUWANOA BENFICA


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Benfica ya Ureno imethibitisha rasmi kumteua José Mourinho (The special one) kuwa kocha wao mpya, akichukua nafasi ya Bruno Lage aliyeondolewa kufuatia kipigo cha mabao 3-2 walichokipata kutoka kwa Qarabag katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, siku ya September 16.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63, raia wa Ureno, aliongoza AS Roma kisha kufanya kazi na Fenerbahce kabla ya kuachishwa majukumu mnamo Agosti 29, 2025 hatua hii inamrejesha Benfica, klabu aliyowahi kuanzia nayo kazi ya ukocha mwaka 2000 kabla ya kuondoka kutokana na mvutano na uongozi wa wakati huo.

Mourinho, nikocha mwenye uzoefu mkubwa akifundisha vilabu vikongwe kama vile akufundisha FC Porto, Chelsea, Real Madrid, Inter Milan, Manchester United na Tottenham Hotspur, amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka klabuni hapo hadi Juni 2027.


Kwa kurejea kwake, Mourinho anatarajiwa kuimarisha kikosi cha Benfica na kurejesha matumaini ya mashabiki baada ya matokeo yasiyoridhisha yaliyosababisha mabadiliko ya benchi la ufundi na anatarajia kuingiza timu hiyo kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya UEFA ambayo wameanza kwa kipigo wakiwa nyumbani.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments