TAOUSSI APEWA MKONO WA KWAHERI HUKO MOROCCO

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Aliyekuwa kocha wa Azam FC, Rachid Taoussi, amejikuta akipoteza ajira mapema katika timu yake mpya ya Kawkab Athletic Club Marrakech (KACM) nchini Morocco, hatua hiyo imechukuliwa na uongozi wa klabu hiyo baada ya kikosi chake kushindwa kupata ushindi katika michezo mitatu ya mwanzo ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26.

Kawkab chini ya Taoussi walipoteza michezo yote mitatu na kupoteza michezo yote Kwa matokeo yafuatayo.

0-1 dhidi ya Wydad

1-2 dhidi ya RS Berkane

1-2 dhidi ya Chabab Dcheira

Matokeo hayo yameonekana kuyumbisha mwanzo wa msimu kwa timu hiyo na kuibua hofu kwa mashabiki pamoja na viongozi wa klabu, hali iliyopelekea uamuzi wa haraka wa kumtimua kocha huyo.


Kwa hatua hiyo, Taoussi anakuwa kocha wa pili kufutwa kazi msimu huu wa ligi ya Morocco, baada ya Lasaad Chabbi kuondolewa Raja Casablanca na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Simba SC, Fadlu Davids.

Hali hii inadhihirisha jinsi ligi ya Morocco inavyokuwa na ushindani mkubwa huku makocha wakipewa presha ya matokeo ya haraka pindi wanapoanza misimu mipya.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments