STARS KUIKABILI BRAZZAVILLE KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2026

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kimeondoka nchini leo kuelekea Congo Brazzaville kwa ajili ya mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 mchezo utakaopigwa septemba 5 mjini Brazzaville.

Safari hiyo imekuja wakati wachezaji wakiwa na morali ya hali ya juu, huku benchi la ufundi likiahidi mapambano makali kuhakikisha Tanzania inaendeleza kampeni zake za kusaka tiketi ya kushiriki michuano mikubwa zaidi duniani.

Kocha mkuu pamoja na wasaidizi wake wameweka wazi kwamba kikosi hicho kipo tayari kupambana vilivyo, wakiamini kwamba ushindi katika mchezo huo wa kwanza utakuwa chachu ya mafanikio makubwa katika hatua ya makundi.

Stars wanashika nafasi ya pili kwenye kundi E wakiwa na alama tisa nyuma ya Morocco wenye alama 15, katika mchezo wa kwanza ulio zikutanisha timu hizo katika dimba la Benjamin Mkapa Stars waliibuka na ushindi wa 3-0, matokeo hayo yanawapa ujasiri na kuingia kifua mbele wakiamini watapata matokea yaliyo bora.

Stars ikipata matokeo mazuri, itajiweka katika nafasi nzuri ya kuendeleza safari yake ya kuwania nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Mashabiki wa soka ndani na nje ya nchi wanatarajia kuona mchezo wa kuvutia, huku matumaini makubwa yakiwa kwamba Taifa Stars itaandika ukurasa mpya wa historia kwenye kampeni za kufuzu Kombe la Dunia 2026.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments