Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Katika ulimwengu wa soka la kisasa, kila dakika na sekunde ina thamani kubwa, muda ndio unaoamua matokeo ya mchezo, kuanzia mwanzo hadi kipenga cha mwisho, Mashabiki wengi wanaona bango la kielektroniki la kubadilishia wachezaji kama chombo cha taarifa tu linaonyesha nani anaingia, nani anatoka na muda wa nyongeza.
Hata hivyo nyuma ya bango hilo kuna hadithi ya kipekee ya ushirikiano kati ya michezo na biashara ya kifahari, ambapo jina "Hublot'' kampuni maarufu ya saa za kifahari kutoka Uswisi, limepata nafasi ya kipekee.
Hublot ilianzishwa mwaka 1980 na Carlo Crocco tangu mwanzo chapa hii ilijitofautisha kwa kuunganisha teknolojia ya kisasa na ustadi wa kutengeneza saa za kifahari. Jina “Hublot” lenyewe linamaanisha “dirisha la meli” kwa Kifaransa, ishara ya mtazamo wa ubunifu na upekee, Miaka ya hivi karibuni, kampuni imejikita sana kwenye michezo, hasa kandanda, kama njia ya kujiunganisha na hadhira kubwa zaidi duniani.
Kwa kupitia ubia huu, Hublot imejijengea nafasi ya kipekee ambapo chapa yake si tu inatambulika na mashabiki wa michezo ya kifahari, bali pia na wapenzi wa kandanda wa kawaida duniani kote.
Moja ya alama kubwa ya uwepo wa Hublot kwenye mchezo wa soka ni bango la kielektroniki la kubadilishia wachezaji, Bango hili hutumiwa na mwamuzi msaidizi wa nne kuonyesha mchezaji anayebadilishwa pamoja na muda wa nyongeza,Pembeni mwa bango hili, jina la "Hublot" limeandikwa kwa uwazi mkubwa.
Kwa mtazamo wa haraka, inaweza kuonekana kama tangazo la kawaida Lakini kibiashara, hii ni moja ya njia bora zaidi za kuunganisha chapa na hisia za mashabiki Kila mara bango linapoinuliwa, kuna msisimko mkubwa, aidha mchezaji nyota anaingia, ama dakika za majeruhi zimeongezwa Kwa hali hiyo, jina la Hublot linajipenyeza moja kwa moja kwenye kumbukumbu za mashabiki.
Hublot imepata nafasi ya kipekee ya kuunganisha ulimwengu wa saa za kifahari na mchezo maarufu zaidi duniani kama soka Kupitia bango la kubadilishia wachezaji, chapa hii imejijengea nafasi katika kumbukumbu za mashabiki kote duniani. Ni mfano bora wa jinsi biashara inaweza kutumia michezo si tu kwa matangazo, bali pia kwa kuunda alama ya kihisia.
Leo hii, kila mara mwamuzi anapoinua bango la Hublot, ulimwengu mzima unakumbushwa kwamba muda ni hazina kubwa ndani na nje ya uwanja.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment