SINGIDA BLACK STARS MABINGWA KAGAME CUP 2025

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Singida Black Stars imeandika historia kubwa katika ardhi ya Afrika Mashariki baada ya kutwaa ubingwa wa Kagame Cup 2025 kwa mara ya kwanza kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal kutokea Sudan katika fainali iliyopigwa uwanja wa KMC complex jijini Dar es Laam.

Shujaa wa mchezo huo hakuwa mwingine bali ni Clatous Chama, kiungo hatari aliyetua akitokea Yanga ,aliyewatesa mabeki wa Al Hilal kwa ubunifu na uwezo wake wa kipekee wa kuchezea mpira Chama alifunga mabao yote mawili ya Singida dakika ya 20' na 57', huku bao la Al Hilal likifungwa na Adelarazig Taha na kuwafanya Singida kuibuka mabingwa.


Kocha Gamondi, aliyekabidhiwa timu hiyo miezi michache tu iliyopita, amethibitisha hadhi yake kama mwalimu mwenye uzoefu mkubwa barani Afrika, Ndoto yake ya kwanza Singida sasa imegeuka kuwa halisi baada ya kuwaletea kombe kubwa, huku akibeba faraja kubwa kutokana na ubora wa Chama aliyeamua matokeo ya fainali hiyo.

Ushindi huu si tu taji bali pia ni tiketi ya kujiamini kwa Singida Black Stars wanapoelekea kwenye kampeni za michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF, Mashabiki na wadau wa soka nchini Tanzania wamefurahia mafanikio haya, wakiamini kuwa huu ni mwanzo mpya wa kutikisa ramani ya soka la Afrika huku mashabiki soka kutoka mkoani Singida wakimpongeza Chama na kumuahidi ushirikiano ndani ya klabu hiyo.


kila la heri kwa Singida Black Stars, kocha wao Gamondi na staa wao Clatous Chama katika safari hii mpya, yenye matumaini, changamoto na fursa kubwa za kusaka mafanikio makubwa zaidi barani Afrika.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments