Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba SC imetoa shukrani za dhati kwa Kocha Hemed Suleiman maarufu kama Morocco baada ya kuiongoza timu hiyo katika mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United na kufanikisha kuivusha hatua ya awali baada ya sare ya 1-1, nakuifanya Jumla ya matokeo kuwa 2-1.
Katika taarifa yao, Simba SC ilieleza kuwa mchango wa Kocha Morocco ulikuwa wa thamani kubwa, hasa ikizingatiwa kuwa aliunganishwa haraka na kikosi hicho, akitokea kwenye majukumu yake ya kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Aidha, Simba ilitoa shukrani kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco kujiunga nao kwa muda mfupi, jambo lililowezesha kikosi hicho kusonga mbele hatua inayofuata.
Hata hivyo, baada ya kukamilika kwa jukumu hilo, klabu hiyo imethibitisha kuwa Kocha Morocco amepewa mkono wa kwa heri rasmi na kurejea kwenye majukumu yake ya Taifa Stars.
Simba SC sasa inaendelea na maandalizi ya mechi zake zijazo chini ya benchi lake la ufundi, huku ikisisitiza mshikamano na malengo ya kufanikisha safari yao .
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com
Post a Comment