SIMBA YAKIRI UDHAIFU MBELE YA YANGA YAPIGIKA MARA SITA MFULULIZO

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezo wa Ngao ya jamii uliowakutanisha mahasimu wa jadi Simba na Yanga katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es laam umetamatika kwa klabu ya Yanga Africans kuibuka na ushindi wa 1-0 bao lililo fungwa na mshambuliaji wao hatari Pacome zouzoua mnamo dakika ya 56'.

Mbali na matokeo hayo klabu ya Simba imeendeleza uteja dhidi ya watani wao baada ya kuruhusu kufungwa michezo sita mfululizo, katika michezo hiyo wamefungwa Jumla ya goli 12 huku wakifunga goli mbili tu kitu kinacho dhihirisha ubora wa Yanga mbele ya mnyama.


Licha ya kupoteza mchezo huo Simba Sc wameonyeshwa kuimarika hasahasa kwenye eneo la ulinzi changamoto ambayo ilikuwa ikiwatesa kwa muda ubora huo umekuja baada ya usajili wa beki kisiki Rushine De reuck ambae anaonekana kuiongoza safu ya ulinzi akishirikiana na Chamou na Hamza.

Baada ya mchezo huo timu nne za Tanzania ambazo ni Simba, Yanga , Azam na Singida black stars zitakwenda kuanza mashindano ya Mechi za kimataifa klabu bingwa na shirikisho mashindano yatako chezwa siku ya tarehe 20 na 21 septemba mwaka huu.

Baada ya mchezo huo wa Ngao ya jamii ligi inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 17 kwa michezo miwili ambapo KMC atawakaribisha Dodoma Jiji huku Costal Union wakiwakaribisha Tanzania prison.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments