SIMBA DAY NGURUMO ZA MNYAMA


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ni mwezi wa nane, tarehe nane, siku ya kipekee kwenye kalenda ya mamilioni ya wapenda soka  si tu Tanzania, bali kote Afrika, hii si tarehe ya kawaida, hii ni simba day siku ya fahari, siku ya mapenzi ya damu, siku ya mnyama mkali kutetemesha taifa kujitambulisha kuelekea msimu mpya.

Maono ya Simba day yalizaliwa mnamo mwaka 2009 , ambapo mpaka sasa wanaadhimisha na kuenzi utamaduni waliouanzisha ambao unawavutia mamilioni ya Mashabiki wa Mnyama na wapenda soka ulimwenguni japo mwaka kuu kutokana na kuingiliana kwa ratiba tarehe ilibadilika na kufanyika septemba 10 ,2025.


Kama simba aingiaye porini kwa mwendo wa kishindo, ndivyo mashabiki wa Simba huvaa rangi nyekundu na nyeupe, wakimiminika kama mto uliovunja kingo, kuelekea kwenye dimba kongwe  la Benjamin mkapa stadium unaweza kupaita lupaso, Kila kona hujaa shangwe, nderemo, na midundo ya burudani inayotikisa anga za jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla mpaka kule safu za milima ya Rungwe,

Simba Day haikuzaliwa kwa mzaha, ilizaliwa kwa dhamira ya kuiunganisha familia ya Simba, kuenzi historia ya utukufu, na kuwatambulisha mashujaa wapya wa vita vya ligi kuu, tangu mwaka 2009, simba day imekuwa tamasha kubwa kuliko yote ya klabu binafsi Afrika Mashariki.

Katika siku hii, historia huzungumzwa kwa lugha ya nyimbo, macho huangua machozi ya furaha na mashabiki huapa kiapo cha uaminifu kwa klabu yao na kwa kuitetea nembo yao, sio Tanzania tu bali mpaka nje ya mipana ya Afrika.



Simba Day si mechi tu, Ni ibada ya soka na uwanja unaogeuka madhabahu, mashabiki kuwa waumini, wachezaji kuwa makasisi, na goli kuwa sadaka ya ushindi.

Wasanii mashuhuri hutumbuiza, wakileta hamasa isiyoelezeka, Rapa huibua sauti ya mtaa, na waimbaji huimba nyimbo za sifa kwa Simba kama mashairi ya jadi yanayosimulia hadithi za mashujaa wa zamani, hapo ndipo jina la kina Mohamed dewij, Mangungu au  Shomari kapombe hutajwa kama majabali wa Simba  walioandika historia kwa jasho na damu.

Wakati Simba Day inasherehekea yaliyopita, haikosi kutazama kesho Kikosi kipya hutambulishwa kwa heshima kubwa , Mchezaji mpya akiingia uwanjani hupewa heshima ya kifalme  si kwa sababu ya jina lake tu, bali kwa matumaini aliyobeba Jezi mpya hutambulishwa, si kama nguo tu, bali kama bendera ya mapambano mapya.

 

Na hapo ndipo mashabiki huapa “Tuko nyuma yenu kwa mvua au jua, kwa ushindi au kipigo, sisi ni Simba damu.”

Simba Day ni ujumbe pia darasa la umoja, uzalendo na mshikamano huwezesha biashara, huamsha vipaji, huunganisha watu wa tabaka mbalimbali ni tamasha linalojenga si tu klabu – bali taifa.

Kwa watoto wanaoota kuwa nyota, Simba Day ni ndoto inayoonekana , Kwa mama sokoni, ni fursa ya biashara, Kwa vijana ni jukwaa la sanaa Kwa Tanzania, ni fahari ya michezo na kivutio Cha utalii.



Simba SC si jina tu, Ni historia, Ni damu, Ni mapenzi yanayovuka mipaka pia ni ishara kuu ya mapenzi baina ya klabu na mashabiki, siku ambayo kila simba mdogo au mkubwa huvuta pumzi kwa nguvu nakusema mimi ni simba na simba ni mimi.

SIMBA NGUVU MOJA.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments