Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Ni siku mpya tarehe 12 September 2025 al ijumaa kareem, asante Mungu tumeliona tena jua ila kwa jua lililopambazuka juu ya anga la Dar es Salaam, kwa mashabiki wa Yanga SC, jua hilo si la kawaida ni taa ya dhahabu inayowaita kushiriki ibada ya kijani na njano pale Lupaso Benjamin mkapa.
Ni Yanga Day, siku ambayo kila moyo wa mwananchi mwenye damu ya kijani hupiga kwa midundo ya shangwe na fahari ni siku ya kuvaa kijani na njano bendera ya yanga ikipepea kuashiria siku muhimu yakuwakutanisha wanchi pamoja kwa lengo la kuwatambilisha na kuwakaribisha nyota wapya katika familia ya Jangwani.
Siku hii uwanja hutikiswa na wimbi la mashabiki, nyimbo zikipaa angani kama mawimbi ya bahari yanayogongana ukingoni mwa miamba bendera zinapeperuka kama mbawa za tai, na kila kijani kinachomulikwa na jua huwa ni alama ya uhai wa klabu kongwe kuliko zote nchini Yanga afrika.
Hii si tu siku ya kuwatambulisha wachezaji wapya kama Doumbia na zimbwe jr, ni hadithi ya kizazi na kizazi, hadithi inayosimuliwa kwa vicheko, nyimbo, machozi na matarajio mapya. Wachezaji wanapokanyaga uwanja kwa mara ya kwanza, ni kana kwamba wamevalishwa joho la kifalme jezi ya kijani na njano ikiwafanya kuwa mashujaa wapya wa taifa, na shangwe nyingi kwa viongozi wa klabu.
Na wakati mchezo wa kirafiki wa Yanga dhidi ya bandari Fc unapoanza, si mchezo tu unaochezwa ni sherehe ya ndoto Kila pasi ni ushairi, kila bao ni fasihi ya heshima, kila mbwembwe ya mchezaji ni mstari mpya katika kitabu kikongwe kilichoandikwa tangu 1935.
Yanga Day ni zaidi ya siku ni kumbukumbu hai, ni chemchemi ya mshikamano, ni urithi unaopita kutoka kwa babu kwenda kwa mjukuu.
Kwa mashabiki wa Yanga, hakuna siku kama hii ni siku ya kujiona si tu mashabiki, bali warithi wa hadithi, walinzi wa heshima, na wapiga mbiu wa ushindi unaokuja ni siku ya kupaza sauti na kusema daima mbele, nyuma mwiko, this is Yanga the pride of Tanzania, Happy wananchi day kwa wanayanga wote.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment