SIFA YA BIGWA NI KUSHINDA BILA KUJALI KACHEZAJE

 Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Siku zote bingwa huanza kuonekana mapema kutokana na jinsi anavyo pata matokeo yake kwenye michezo mbali mbali kwa kushinda Kila mchezo bila kujali amecheza vizuri au vibaya huo ndio utambulisho wa timu yenye sifa ya kuwa bingwa.

Katika ligi kuu nchini England sifa za bingwa zimeanza kuonekana kwa klabu ya Liverpool baada ya Jana kuendeleza ubabe wakiwa ugenini kwa kuichapa Burney kwa bao 1-0 licha ya kucheza kawaida ila muhimu ilikuwa ni alama tatu .

Baada ya mchezo wa Jana Liverpool wanazidi kujikitankileleni mwa msimamo wakiwa na alama 12 huku wakifuatiwa na Arsenal na Tottenham wenye alama 9 kwenye michezo minne lakini wapinzani wa Liverpool kama Chelsea na Man city ambao wanatarajiwa kutoa changamoto wamesha dondosha alama kwenye michezo kadhaa huku Chelsea wakitoa sare ya 2-2 na Brentford nakuzidi kuweka pengo dhidi ya mpinzani wao Liverpool.

Ikumbukwe Liverpool ndio mabingwa watetezi wa premier league na sasa wanaonekana kuendelea walipo ishia, kinacho kwamisha vilabu vingi Kutwaa taji hili EPL ni namna wanavyo poteza alama kwenye michezo ya mwanzoni lakini kwa majogoo imekuwa tofauti wamezidi kuonyesha kuwa wanania ya Kutwaa ubingwa bila kujali wanachezaje.

Washindani wa Liverpool kama Man city, Arsenal,Chelsea na Tottenham wataendelea kupoteza alama na Liverpool washinde michezo yao huenda ukawa msimu ambao bingwa atapatikana mapema ila kama vilabu hivyo vinataka vionyeshe ushindani inabidi vihakikishe havidondoshi alama hovyo.

0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments