SARE YA MAN CITY NA ARSENAL, NEEMA KWA LIVERPOOL

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Pengo la alama katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England limezidi kuwa kubwa baada ya miamba wawili, Manchester City na Arsenal, kulazimishana sare ya 1-1 kwenye mchezo wa mzunguko wa tano EPL jana kwenye dimba la Emirates



Matokeo hayo yameonekana kuwa habari njema kwa Liverpool, ambao sasa wamejiongezea nafasi kubwa zaidi kileleni mwa msimamo wa ligi , Kwa sare hiyo, City na Arsenal wote wamedondosha alama mbili katika mchezo huo na kumruhusu Liverpool kuendeleza uongozi wao kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya timu zinazomfuatia ambazo ni Arsenal, Tottenham na Bournemouth wakiwa na alama kumi Kila mmoja.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa soka, sare hii imekuwa pigo kwa wapinzani hao wakubwa wa moja kwa moja wa Liverpool, kwani kila mmoja alikuwa na matarajio ya kupunguza pengo la alama na kujiweka katika nafasi ya ushindani mkali zaidi.


Hali hiyo sasa inaiweka Liverpool kwenye nafasi nzuri ya kuutafuta ubingwa msimu huu ikizingatiwa mpaka sasa hajadondosha alama  ikichagizwa na ubora wa kikosi chao na mwenendo mzuri wa matokeo waliyo nayo hadi sasa.

Wana Anfield wanaonekana kuwa na kila sababu ya kufurahia, huku wapinzani wao wakuu wakizidi kudondosha alama muhimu katika mbio hizi za kusaka taji la ligi kuu England huku kama Hali ikiendelea kuwa hivyo huenda bingwa akapatikana mapema kinyume na matarajio ya wengi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments