SAFARI TA STARS KOMBE LA DUNIA YATAMATIKA


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) rasmi hawatashiriki kombe la Dunia mwaka 2026 litakalo fanyika  nchi za Marekani, Mexico, na Canada, baada ya kukubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa Niger kwenye mchezo uliopigwa dimba la New Aman visiwani Zanzibar kitu kilicho zima ndoto na matumaini ya stars kuelekea kombe la Dunia.

Stars walitarajiwa kufanya vizuri kwa kuwa na alama nyingi katika nafasi ya pili ili kupata nafasi ya kucheza bestlooser (timu yenye alama nyingi nyuma ya anae ongoza kundi) lakini baada ya mchezo huo wamesalia na alama 10 na michezo saba nyuma ya Morocco wenye alama 21, huku wakisalia na mchezo mmoja .

Katika kinyang’anyiro cha bestlooser zinahitajika timu nne pekee ili kutafuta timu moja lakini kwa alama walizo kuwa nazo stars imekuwa ngumu kwa sababu kwenye msimamo wa washindi wa pili wenye alama nyingi  Stars inashika nafasi ya tisa na alama kumi huku nafasi ya kwanza mpaka ya nne zinashikiliwa na Gaboni alama 19, Madagascar 16, DR Congo alama 16 pamaoja na Burkina Faso alama 15.



Baada ya matokeo hayo mijadala iliibuka huku wachambuzi na wadau wa soka nchini wakiomba kubadilishwa kwa benchi la ufundi kwa kuleta makocha wenye uwezo na uzoefu Zaidi ya waliopo sasa wamebainisha kuwa Tanzania kuna vipaji vikubwa lakini tatizo linakuja kwenye uwezo wa kimbinu.

Ikumbukwe katika michezo miwili ya mwisho ya kufuzu kombe la Dunia Stars walicheza chini ya kiwango ukilinganisha na uwezo wawachezaji wa timu hiyo, utengenezwaji wa nafasi ulikuwa wa chini pia timu ilikosa utulivu wakati wa mchezo, katika mchezo uliopita Niger walicheza pungufu takribani dakika 15 lakini stars bado hawakutengeneza nafasi za kusawazisha makosa yao.

Kwa upande wake kocha Hemed Suleiman amesema kuwa walijitahidi kuingia kwenye mchezo huo kwa kupata goli la mapema lakini kutokana na uchovu wa wachezaji walishindwa kutengeneza nafasi licha ya kufanya mabadiliko kadhaa lakini bado haikubadilisha kitu, kwa sasa wanarudi na kurekebisha changamoto hizo.

Stars watakamilisha ratiba ya mashindano hayo dhidi ya Zambia na sasa wachezaji wanarejea kwenye vilabu vyao ili kuendelea na maandalizi ya ligi.

0767915473,

Lugembetimothy01@gmail.com

 

 

0/Post a Comment/Comments