Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kipa wa Manchester United, Andre Onana, amekubali kujiunga na klabu ya Uturuki, Trabzonspor, kwa mkopo, Ingawa uhamisho huo bado haujakamilika, vyanzo vya karibu na mchezaji huyo vinatarajia utamalizika kabla ya Jumapili tarehe 14 Septemba, ili aweze kufanya mchezo dhidi ya Fenerbahce.
Dirisha la usajili Uturuki linabaki wazi hadi Ijumaa, jambo linalotoa nafasi ya kukamilisha mpango huo huku Onana akiwa kwenye majukumu ya kimataifa na timu yake ya Taifa Cameroon.
United kwa sasa ina makipa wanne wakuu Onana, Altay Bayindir, Tom Heaton na Lammens, ingawa viongozi wa klabu walisisitiza wako tayari kubaki na makipa wanne, kocha Ruben Amorim ametaka kuwa na kikosi kidogo kutokana na ukosefu wa michezo ya Ulaya, nakuifanya nafasi ya onana kuwa finyu kikosini hapo.
Onana alihitimisha msimu uliopita akiwa kipa namba moja wa United baada ya kuanza katika fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham ,hata hivyo, jeraha la msuli wa paja mwanzoni mwa maandalizi ya msimu lilimnyima nafasi ya mechi za kirafiki na michezo mitatu ya kwanza ya Premier League, ambapo Bayindir alipewa nafasi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alisajiliwa kutoka Inter Milan kwa dau la pauni milioni 47.2 mwaka 2023, chini ya Erik ten Hag aliyekuwa anamtambua tangu Ajax.
Hata hivyo, Onana hajawahi kuonekana akiwa na utulivu mkubwa na mara nyingi amekuwa akikosolewa baada ya makosa ya mara kwa mara.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment