NYOTA WAPYA WALIOTIKISA SIMBA DAY


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba Sc imefanya tamasha lake la 17 toka mwaka 2009 siku ya jana septemba 10, 2025 lengo likiwa ni kutambulisha kikosi chake kwa msimu ujao , ambapo walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor mahia kutoka nchini Kenya ambapo waliibuka na ushindi wa 2-0, mabao yaliyofungwa na Hamza 7’ pamoja na Mukwala 49’.

Katika mchezo huo  mashabiki na wadau wa soka nchini macho na masikio yao yalikuwa ni kutazama uwezo wa wachezaji wao wapya walio wasajili katika mchezo huo nyota wapya waliopata nafasi ya kucheza ni pamoja na Sowah, Naby Camara, Neo Maema, Mlingo, De reuck, Mligo, Kante, Morice ,pamoja na Mwalimu.

Katika wachezaji hao wapya wachezaji walio onyesha kiwango kilicho wavutia wadau mashabiki na wadau wa soka ni pamoja na De reuck, Naby Camara, pamaja na Morice .

DE REUCK


Huyu ni beki wa kati aliesajiliwa kutoka Mamelod sundown katika mchezo wa jana ameonyesha kiwango bora Zaidi katika eneo la ulinzi kutokana na utulivu mkubwa wakati akiwa na mpira , uwezo wake wa kupiga tackling kwa usahihi, hajasubiria michezo mingi ili kudhihirisha uwezo wake, kama majeraha yasipo muandama basi ni msaada mkubwa sana kwa mnyama kuelekea msimu ujao.

NABY CAMARA


Ni mchezaji ambae anauwezo wa kucheza maeneo tofauti tofauti uwanjani akisifika kwa ubunifu wake katika mchezo wa jana Camara alionekana kucheza kama mchezaji huru akigusa kila eneo kitu kilicho onyesha uwezo wake wa kucheza sehemu tofauti tofauti , mbali na hilo anauwezo wa kuchuku mpira kutoka kwenye nusu ya samba na kuanzisha mashambulizi kwenda kwa wapinzani .

MORICE ABRAHAM



Ni mchezaji kijana wa ki Tanzania ambae aliingia kipindi cha pili anacheza kama namba 10 ambapo kwa muda aliocheza alionyesha uwezo wake wa kukaa na mpira pia kupiga mashuti , kama akipewa nafasi na kuongeza juhudi mchezaji huyu ataonyesha kiwango bora.

Hii ni tathmini fupi tu kwa mchezo tu mmoja haimaanishi hawa ni wachezaji bora kuliko waliosajiliwa bali kwa mchezo wa jana hawa ndio waliwavutia mashabiki na wadau wa soka hata hivyo usajili wa msimu huu uliofanywa na Simba Sc umeonyesha nia yao madhubuti ya kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali na msimu huu dhana ya kikosi kipana imeonekana ndani ya klabu hiyo.

0767915473,

Lugembetimothy01@gmail.com.

 

                                                                                                              

0/Post a Comment/Comments