NDOA YA SIMBA NA FADLU MATATANI


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Hali ya sintofahamu imezidi kuikumba klabu ya Simba SC baada ya taarifa kuibuka kwamba Kocha Mkuu wao, Fadlu Davids, yupo kwenye hatua za mwisho za kuondoka na kujiunga na moja ya timu kubwa nchini Morocco.

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa Davids amepokea ofa ya kuvutia kutoka klabu ya Morocco, ikiwa ni pamoja na mshahara mara tatu ya kile anacholipwa kwa sasa na Simba SC, Hali hiyo imeifanya Simba kukumbwa na wakati mgumu wa kumbakiza kocha huyo ambaye kwa mujibu wa vyanzo, ameshajipanga kuondoka pamoja na benchi lake lote la ufundi.


Inadaiwa kuwa usiku wa kuamkia leo, Raja Casablanca walitangaza kutimua kocha wao, jambo ambalo linaongeza uwezekano mkubwa wa Fadlu kuchukua nafasi hiyo, Uamuzi huo unatajwa kuwa ni moja ya sababu zinazomhakikishia nafasi kubwa katika klabu hiyo maarufu ya Morocco.

Ripoti zaidi zinaonyesha kwamba Simba tayari imeanza mchakato wa kutafuta mrithi wa mikoba ya Fadlu, huku ikijipanga kwa maisha mapya bila kocha huyo ingawa klabu hiyo imejaribu kwa jitihada kubwa kumbakiza, dalili zote zinaashiria kuwa safari yake nchini Tanzania inakaribia mwisho.

Kuna matarajio kwamba baada ya mechi ya leo, taarifa rasmi huenda ikatolewa hadharani kuthibitisha mwelekeo mpya wa Fadlu Davids na mustakabali wa Simba SC kwenye benchi la ufundi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments