Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi kuwa hafla kubwa ya utoaji wa tuzo kwa wachezaji na wadau walioweka historia na kufanya vizuri kwenye soka la ndani, maarufu kama TFF Awards 2025, itafanyika mapema mwezi Desemba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo, tukio hilo litaambatana na utoaji wa tuzo mbalimbali zinazotambua mafanikio katika mashindano ya ndani kwa msimu wa 2024/2025. “Tarehe kamili ya hafla hiyo itatangazwa mara baada ya maandalizi kukamilika,” imesema sehemu ya taarifa ya TFF.
Tuzo hizo zitagusa makundi kadhaa ikiwemo Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB, Ligi Kuu ya Wanawake, Ligi ya NBC Championship, First League, pamoja na Ligi ya vijana ya U20 inayodhaminiwa na NBC, Pia kutakuwa na tuzo za kiutawala ambazo hufahamika kwa kutoa heshima kwa viongozi na wadau waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya soka nchini.
Hamu na matamanio makubwa ya wadau ni kutangazwa kwa Mchezaji Bora wa Msimu (MVP) kwa mwaka 2024/2025, ambaye atapigiwa kura na kupendekezwa kutokana na mchango wake mkubwa ndani ya uwanja pia TFF imethibitisha kuwa wachezaji, viongozi na wadau kutoka sehemu mbalimbali watashuhudia hafla hiyo, huku Serikali na wadhamini wakuu wakihusishwa moja kwa moja.
Kwa miaka ya karibuni, hafla za utoaji tuzo za TFF zimekuwa kivutio kikubwa si tu kwa wapenzi wa soka, bali pia kwa jamii nzima kutokana na heshima inayotolewa kwa nyota wanaoibeba taswira ya michezo nchini, mwaka huu inaonekan tuzo zinaenda kukosa mvuto kwasababu ya uchelewashwaji wa kutolewa kwa tuzo hizo kutokana na mwingiliano wa ratiba ikiwemo mashindano ya CHAN.
Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu kuona ni nani atakayeibuka na tuzo kubwa zaidi, huku majina kama Ahoua na Pacome yakiwa MStari wa mbele Kutwaa tuzo hiyo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment