MICHEZO MIWILI IMETOSHA KUMUONDOA TEN HAG LEVERKUSEN


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Aliyekuwa kocha mkuu wa Bayer Leverkusen, Erik Ten Hag, amepata mshangao baada ya kuondolewa kazini na uongozi wa klabu hiyo ndani ya muda mfupi wa msimu mpya kuanza,Ten Hag alitimuliwa baada ya kuiongoza Leverkusen kwenye michezo miwili pekee ya Ligi, jambo ambalo ameliita la kushangaza na lisilo na maelezo ya kina.

Akizungumza mara baada ya uamuzi huo, Ten Hag alisema

"Nimeshangazwa sana na uamuzi wa Uongozi wa klabu ya Bayer Leverkusen kwa kunifuta kazi baada ya michezo miwili tu ya Ligi ni jambo la kushangaza sana."

Kocha huyo aliongeza kuwa mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha Leverkusen ndiyo yaliyosababisha ugumu wa kupata matokeo ya haraka, hasa baada ya wachezaji muhimu kuondoka majira ya kiangazi.

"Majira haya ya kiangazi, wachezaji muhimu wengi waliokuwa sehemu ya mafanikio ya nyuma waliondoka kwenye kikosi, Kujenga timu mpya ni mchakato unaohitaji muda na imani," alisema Ten Hag.

Pia alitoa wito kwa kocha atakayekabidhiwa mikoba hiyo kupewa nafasi ya kutekeleza falsafa zake bila presha ya matokeo ya haraka.

"Kocha mpya anastahili nafasi ya kuweka maono yake, kusimamia viwango, kuunda kikosi, na kuacha alama yake katika mtindo wa uchezaji," aliongeza Ten Hag

Katika michezo miwili waliyocheza katika ligikuu ya Ujerumani wamepoteza mchezo mmoja na kutoa sare mchezo mmoja matokeo ambayo yanawafanya washike nafasi ya 12 wakiwa na alama moja, jambo ambalo limewafanya viongozi wa klabu hivyo kufanya maamuzi magumu na yamapema.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments