Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mashabiki wa timu ya taifa ya DR Congo walijikuta wakifanya vurugu kwa kung’oa viti katika mchezo wao dhidi ya Senegal wa kufuzu kombe la Dunia 2026 uliopigwa Kinshasa nchini Congo.
Katika mchezo huo DR Congo walitangulia mbele kwa mabao mawili yaliyo wekwa kimiani na Cedric Bakambu 27’ na Yoane Wissa 33’ baada ya uongozi huo mashabiki wa Congo waliamini wameimaliza mechi lakini isivyo bahati Senegal walikuja juu na kusawazisha makosa yao kwa kufunga magoli matatu yalifungwa na Pape Gueye 39’ , Nicolas Jackson 53’ na msumali wa mwisho ukipigiliwa na Pape Sarr 87’ na kuufanya mchezo kutamatika kwa DR Congo kupoteza kwa bao 3-2 wakiwa nyumbani.
Baada ya mchezo huo Senegal anapanda nafasi ya kwanza na alama 18, akifatiwa na DR Congo alama 16 huku kila timu ikisalia na michezo miwili kuelekea kukamilisha ratiba ya michuano hiyo.
07679155473,
Lugembetimothy01@gmail.com
Post a Comment