Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports
"TABIA NI KAMA NGOZI HAIBADILIKI KIRAHISI ,TIMU YA LIVERPOOL IMEZIDI KUISHI TABIA YAKE YA KUSHINDA DAKIKA ZA JIONI BAADA YA HAPO JANA KUPATA USHINDI DAKIKA YA 85' KUPITIA EKITIKE HUKU MATUKIO YA KADI NYEKUNDU KWA EKITIKE NA BAO LA ISAK VIKINAKSHI MCHEZO"
Liverpool imeendelea kuonyesha tabia ya kupata ushindi katika dakika za lala salama baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Southampton kwenye dimba la Anfield katika mchezo wa Carabao Cup.
Katika mchezo huo mabao ya Liverpool yaliwekwa kimiani na Alexander Isak 43' na Hugo Ekitike 85' huku bao la kufutia machozi la Southampton likiwekwa kambani na Shea Charles 76'. Kwa ushindi huo unaendeleza desturi ya Liverpool msimu huu kupata ushindi katika dakika za ukingoni.
Katika hatua nyingine mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa dau kubwa la pauni milioni 125, Alexander Isak, aliwapa mashabiki wa Anfield ladha ya ubora wake kwa kufunga bao safi katika mchezo wake wa pili tu tangu ajiunge akitokea Newcastle, Hata hivyo, alitolewa mapumziko ya kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Hugo Ekitike, ambaye ameanza msimu kwa moto wa mabao.Ekitike, ambaye tayari ana mabao matatu kwenye ligi, alionyesha tena ubora wake kwa kufunga bao la ushindi, ingawa shangwe zake zilimgharimu baada ya kuvuliwa jezi na kuonyeshwa kadi nyekundu ya pili, hali hiyo imewapa mashabiki uhakika kuwa Isak atapata nafasi ya kuendelea kuonyesha makali yake katika mchezo unaofuata dhidi ya Crystal Palace.
Kwenye upande mwingine, Federico Chiesa aliangaza kwa ustadi wake, akitoa pasi mbili za mabao na hata kufunga goli lililokataliwa kwa kuotea, jambo lililosisitiza mchango wake kwa kikosi cha Liverpool.
Kwa Southampton, mambo bado ni magumu chini ya kocha Will Still, timu hiyo imeshinda mchezo mmoja pekee msimu huu na inabaki juu kwa pointi mbili tu dhidi ya hatari ya kushuka daraja.
Hata hivyo, Southampton walikaribia kupata bao muhimu pale shuti la Adam Armstrong lilipogonga mwamba kabla ya mpira wa kichwa wa Leo Scienza kupaa juu, sekunde chache tu kabla ya Isak kufungua ukurasa wa mabao yake Anfield.
Liverpool sasa inaendelea kubaki na kasi ya ushindi, huku mashabiki wakingoja kuona iwapo Isak ataweza kuonyesha thamani ya pesa alizonunuliwa kwa kuendeleza makali yake katika mechi zijazo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment