LIVERPOOL YAWEKA REKODI KWA ISAK


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Liverpool imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alexander Isak kwa ada ya pauni milioni 125, rekodi kubwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu England, Nyota huyo wa Sweden amejiunga rasmi akitokea Newcastle United baada ya mzozo wa muda mrefu uliokuwapo kati ya mchezaji huyo na klabu yake ya zamani.

Kwa muda mrefu Isak alikuwa akihusishwa na kuondoka St. James’ Park, huku ripoti zikieleza kuwa hakuridhishwa na mwelekeo wa Newcastle licha ya ubora aliouonyesha msimu uliopita hatimaye Liverpool imefanikiwa kumpata, ikimpa mkataba wa hadi Juni 2031, jambo linalodhihirisha dhamira ya klabu hiyo ya kuimarisha safu ya ushambuliaji.

Isak, ni mchezaji mwenye uwezo wa kipekee wa kufunga na kumiliki mpira, msimu uliomalizika alifanikiwa kufunga mabao 23 na pasi za usaidizi 6 katika ligi hiyo ,Kasi yake, uhodari wa kumalizia mashambulizi, pamoja na uwezo wa kucheza kama straika huru, vitakuwa silaha kubwa kwa kikosi cha Liverpool .

Kwa mashabiki wa Liverpool, usajili huu ni ishara ya mafanikio kwenye kupigania makombe makubwa msimu huu, Wengi wanaamini Isak ndiye kipande kilichokosekana kwenye safu ya ushambuliaji ya majogoo hao na anaweza kuwa nyota wa kuandika historia mpya pale Anfield.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments