Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports
Mashabiki wa soka ulimwenguni kote wameendelea kushuhudia upepo mpya unaovuma Anfield, ambapo Liverpool imekuwa na tabia ya kipekee ya kusaka ushindi katika dakika za mwisho Wakiwa wamefanya hivyo katika michezo minne ya hivi karibuni.
Hali hiyo ilijitokeza Jana kwenye mchezo wa UEFA dhidi ya Atletico Madrid ambapopaka dakika ya 90 mchezo ilikuwa sare ya 2-2 lakini ilivyo desturi ya Liverpool kwa siku za hivi karibuni mnamo dakika ya 90+2 Van Dijk aliifungia klabu hiyo bao la tatu na la ushindi lililo kamilisha mchezo wa kupata alama zote tatu kwa ushindi wa 3-2 wakiwa uwanja wa nyumbani Anfild.
MICHEZO WALIYO SHINDA DAKIKA ZA MWISHO
Burnley 0-1Liverpool
Mbali na mchezo huo wa Jana pia hali kama hiyo ilitokea Katika mchezo EPL dhidi ya Bunrey wakiwa ugenini Liverpool waliibuka na ushindi wa 1-0 bao lililofungwa kwa mkwaju wa penalty 90+5 na mshambuliaji Mohamed Salah.
Newcastle 2-3 Liverpool
Mchezo huu uliopigwa uwanja wa St. james'park ambapo mpaka dakika 90 mchezo ulikuwa sare ya 2-2 lakini katika dakika za nyongeza 90+10 Liverpool ndipo walipo pata ushindi wao kwa kupachika bao la tatu kupitia kwa Rio Ngumoha.
Liverpool 4-2 Bournemouth
Mchezo huu uliopigwa katika dimba la Anfild ambapo Liverpool walitangulia kwa 2-0 lakini baadae Bournemouth walisawazasha goli zote kupitia kwa Semenyo wakati mashabiki wakiwa wanaiona sare katika mchezo huo ndio wakati ambao Liverpool walikwenda kuandikisha ushindi kwa mabao ya Chiesa 88' na Salah 90+4 na kuhitimisha ushindi wao katika dakika za mwisho kabisa.
Katika michezo hiyo Liverpool wamekuwa walitangulia kwa goli mbili lakini baadae wanasawazishiwa na kupata ushindi dakika za jioni hali hii imekuwa ikiwatisha mashabiki wa timu hiyo na kuwafikirisha kuwa iwapo siku wanashindwa kupata matokeo kwenye dakika hizo za mwisho inamaanisha watapoteza alama.
Timu zinazocheza na Liverpool zinatakiwa kuwa makini zaidi katika michezo Yao hazitakiwi kubweteka zinatakiwa kucheza mpaka tone la mwisho maana kwa sasa kwa upande wa Liverpool pool haiishi mpaka iishe.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment