LICHA YA MATOKEO MAZURI BADO HAWAMUELEWI

Timothy Lugembe

Mwanakwetusports.

Mashabiki wa klabu ya Yanga wanaonekana kutoridhishwa na uchezaji wa timu yao kitu ambacho kinamuweka matatani kocha wao Romain Folz, mashabiki wa klabu hiyo wanamshutumu kocha huyo kucheza mpira usiovutia.

Mashabiki wanadai kuwa kocha amekuwa akicheza direct football mpira ambao hauna ufundi ukilinganisha na waliyokuwa wamezoea wao Kwa misimu kadhaa ambapo mpira wa kuvutia klabuni hapo ulianzishwa na Kocha Naby ambae alitambulisha soka la kuvutia klabuni hapo kama Wengi wanavoliita pila biriani.


Katika michezo tisa aliyocheza mpaka sasa kashinda yote huku akifunga mabao 20 na kuruhusu goli mbili pekee, hiki ni kiwango cha hali ya juu alicho onyesha kocha huyo lakini licha ya yote hayo Bado anaonekana hatoshi kwenye viatu vya wananchi.

Huenda baada ya mchezo wao dhidi ya Mbeya city siku ya September 30 majibu yakaanza kutoka kuhusu mustakabali wankocha huyo katika mitaa ya twiga na jangwani.


0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments