KWAHERI FADLU DAVIS

Timothy Lugembe ,

Mwanakwetusports.

Kocha raia wa Afrika Kusini, Fadlu Davis, ameondoka rasmi kwenye benchi la ufundi la klabu ya Simba SC na kuelekea nchini Morocco kwa mazungumzo na uongozi wa klabu ya Raja Casablanca.

Habari kutoka vyanzo vya kuaminika  zinasema kuwa Davis amesafiri kwenda Casablanca kukutana na bodi ya Raja Athletic, huku Simba SC wakibaki chini ya uongozi wa kocha msaidizi Suleiman Matola mpaka pale watakapo mtangaza kocha mpya.

Fadlu, ambaye alijiunga na Simba SC kwa muda mfupi, amekuwa na mchango mkubwa katika kurejesha uimara wa kikosi hicho Chini ya uongozi wake alifanya mambo mengi ikiwemo.

-Simba SC ilionekana kurejea katika kasi ya ushindani kwenye Ligi Kuu Bara

-Alisaidia timu kufanya vizuri katika mashindano ya CAF ikiwemo kufika hatua ya fainali ambapo walikubali kichapo dhidi ya RS Berkane kwa Jumla ya 3-1.


Aliwaimarisha wachezaji kadhaa wenye vipaji chipukizi na kuwapa nafasi uwanjani wachezaji kama Chasambi, Barua, na Valentine Mashaka.

-Aliboresha nidhamu na mbinu za kisasa za ufundishaji ndani ya kikosi Cha timu hiyo.

-Alifanikiwa kuipa Simba SC matokeo ya kuvutia dhidi ya wapinzani wakubwa katika mechi muhimu licha ya ujenzi wake wa timu lakini timu ilionyesha uwezo wa juu kiupambanaji.

-Alileta mshikamano na ari mpya kwenye timu  baada ya Timu kupoteana kwa takribanii misimu mitatu alikuja na kuanza kuijenga timu upya japo kuwa hakufanikiwa Kutwaa taji lakini timu ilionekana kuimarika.

Kwa kuondoka kwake, mashabiki wa Simba SC wamesalia na kumbukumbu nzuri ya mafanikio yake, japokuwa muda wake jijini Dar es Salaam ulikuwa mfupi  Safari ya Fadlu kuelekea Casablanca inafungua ukurasa mpya wa mafanikio yake katika soka na kuandika historia nyingine, huku Simba ikibaki na matumaini chini ya Suleiman Matola wakati wakisubiria kutangazwa kocha mpya.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments