Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezo wa ufunguzi wa pazia la Ligi kuu Tanzania Bara ( Ngao ya jamii) unatarajiwa kupigwa kesho septemba 16 katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es laam mchezo utakao wakutanisha wapinzani wa jadi nchini Simba na Yanga.
Kuelekea mchezo huo kumekuwa na mitazamo mingi hasa baada ya Kila timu kumtambulisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa mashindano, kabla ya mchezo unaotarajiwa kupigwa kesho timu hizi zimecheza michezo kadhaa lakini michezo iliyo fatiliwa kwa ukaribu ni siku ya matamasha yao.
SIMBA VS GOR MAHIA
Mchezo huu ulimalizika kwa Simba kushinda bao 2-0, katika mchezo huo kocha wa klabu hiyo Fadlu alionekana kucheza mchezo wa kumiliki mpira zaidi huku katika mfumo anatarajia kutumia msimu huu ni 4-4-2 akiwa anahitaji kutumia washambuliaji wawili ambapo kwa mfumo huo inatarajiwa mchezaji mmoja kati ya Sowah na Mwalimu ataanza kucheza na Mukwala.
Huo ni mfumo lakini kocha anaweza kubadilisha mbinu kutokana na mchezo husika, kutokana na kikosi kipana walicho nacho Simba kwa msimu huu wataleta upinzaninkwa Yanga tofauti na misimu kadhaa nyuma kwakuwa sasa timu inaonekan kuwa imara ila muunganiko Bado haupo kwa silimia miamoja kwenye kikosi hicho.
YANGA VS BANDARI
Mchezo ulimalizika kwa Yanga kushinda 1-0, huku radha ya kiuchezaji ikiwa sio ile iliyozoeleka. katika mchezo huo Yanga walionekana kutumia mabeki watatu nyuma huku idadi ya viungo ikiwa kubwa eneo la katikati ya uwanja hiyo ikimaanisha kuwa silaha Yao kubwa itakuwa katikati ya uwanja.
Kikosi Cha wananchi kinaonekana bado hakuna muunganiko baada ya maingizo mapya kwenye baadhi ya maeneo hasa hasa kati kati mwa uwanaja, ikumbukwe Khalid Aucho alikua kiungo kizuri kilicho unganisha timu kuanzia katikati ya uwanja kwenda mbele na timu nzima ilicheza kwa kumuangalia yeye kwa sasa timu imepoteza mtu kama huyo na inailazimu klabu hiyo kukaa kwa muda sasa ikihitaji kikosi kizoeane kiuchezaji.
WACHEZAJI WA KUANGALIWA ZAIDI
Kwa upande wa Yanga mchezaji wa kuchungwa zaidi ni Pacome zouzoua anaesifika kwa uwezo wa kukaa na mpira muda mrefu, uwezo wa kupunguza wachezaji mpaka wa tatu na kutoa pasi za mwisho kuonyesha kuwa huyu ndie mchezaji hatari zaidi mchezo uliopita hakucheza kabisa kuashiria kuwa ni silaha inayo tarajiwa kutumika kikamilifu hapo kesho.
Kwa upande wa Simba ni Mpanzu na Naby Camara, Mpanzu ni mchezaji mwenye Kasi mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi akitokea pembeni kwa muktadha huohuo licha ya ugeni wake kikosini Naby Camara anatariwa kuwa mchezaji muhimu hasa kwenye utengezaji wa nafasi ambapo anauwezo wa kupiga pasi za hatari , kukuta mipira kuelekea kwa wapinzani pia nauwezo wa kucheza maeneo tofauti tofauti ya uwanja mchezaji huyu atakuwa hatari kama kocha Fadlu atamwachia acheze kama mchezaji huru uwanjani.
TAKWIMU KUELEKEA MCHEZO
Katika michezo mitano ya mwisho waliyo kutana Yanga wameshindwa michezo yote huku wakifunga Jumla ya mabao 11 na kuruhusu goli 2 pekee, hii inaonyesha kuwa hivi karibuni Simba amekuwa akiruhu mabao huku mchezo wa mwisho wakufunga msimu Yanga alipata ushindi wa 2-0.
Katika mchezo wa soka takwimu zinawekwa kama historia tu, na historia zimewekwa ili zivunjwe kwa maana hiyo mchezo wa watani wa jadi hautabiliki dakika tisini ndizo zitakazo muamua mshindi katika mchezo huo huku klabu ya Simba ikiingia kama timu ya pili huku nafasi kubwa yakushinda ikipewa klabu ya Yanga Africa.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.

.jpg)

Post a Comment