KIZUNGUMKUTI: FOUNTAIN GATE WAOMBA MICHEZO YAO KUPELEKWA MBELE

Timothy Lugembe

Mwanakwetusports

Uongozi wa Fountain Gate FC umetangaza ufafanuzi rasmi kufuatia changamoto zilizojitokeza katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, Septemba 18, 2025 ambapo walikubali kipigo Cha 1-0 katika uwanja wa nyumbani Tanzanite kwaraa.

Katika taarifa yao kwa umma, klabu hiyo imeeleza kuwa ililazimika kushuka dimbani ikiwa na idadi ndogo ya wachezaji kutokana na tatizo la kiufundi lililotokana na mfumo wa usajili wa kimataifa (TMS) Licha ya kufuata taratibu zote, usajili wa baadhi ya wachezaji wapya haukukamilika kwa wakati.

Aidha, Fountain Gate imesisitiza kuwa changamoto hiyo imetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa klabu na tayari juhudi za pamoja kati yao na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zinaendelea ili kupata suluhu la kudumu.

Hali hiyo imeathiri maandalizi ya timu, hasa kutokana na idadi ndogo ya wachezaji waliothibitishwa kucheza huku baadhi wakikumbwa na changamoto za kiafya na majeraha Kufuatia mazingira hayo, klabu hiyo imeiandikia Bodi ya Ligi (TPLB) kuomba ratiba ya michezo yao isogezewe mbele hadi pale suluhu litakapopatikana.

Fountain Gate FC imetambua umuhimu wa ushiriki wenye ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara, na imesisitiza kuwa kwa kushirikiana na TFF pamoja na TPLB, watapata mwafaka wa haraka ili kuruhusu kikosi kamili chenye ushindani kushiriki ligi.

Ikumbukwe msimu uliopita timu ya Tabaora united ilikumbwa na mkasa kama huu kwenye mchezo wao dhidi ya Azam fc ambapo awalikubali kichapo Cha bao 4-0 na mwamuzi alilazimuka kumaliza mchezo kabla ya muda kutokana na kanuni zinanoelekeza kuhusu idadi ya wachezaji uwanjani.

Hali hii imejitokeza kwa Fountain gate, hii inaonyesha maandalizi yanakuwa yapi chini sana kuelekea msimu hivyo vilabu vingine vichukue hii kama changamoto wahakikishe katika maandalizi Yao yakamilike asilimia mia sio kiuchezaji tu pia mpaka kufatikia hati zinazo ruhusu wachezaji kucheza.

Hata hivyo Uongozi wa klabu hiyo umewaomba wadau na mashabiki wake kuendelea kuwa wavumilivu na kuipa timu hiyo sapoti katika kipindi hiki cha mpito.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments